- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KESI YA KUBENEA BADO KIZUNGUMKUTI
DODOMA: MAHAKAMA ya Wilaya ya Dodoma imepiga kalenda kesi ya Mbunge wa Ubungo SAED KUBENEA hadi Agosti23 Mwaka huu kutokana na uchunguzi wa kesi hiyo kutokamilika.
Mbunge huyo anashitakiwa Kwa kosa la jinai ambalo anadaiwa kumshambulia Mbunge wa viti maalum JULIANA SHONZA.
Akisoma kesi hiyo leo mbele ya Mahakama hiyo,wakili wa Serikali FOIBE MAGILI amesema kuwa uchuguzi wa kesi hiyo haujakamilika na hivyo kumuomba Hakimu JAMES KARAYEMAHA aisogeze mbele.
Kwa upande wake Hakimu JAMES KARAYEMAHA aliridhia ombi la wakili wa Serikali na hivyo kuiahirisha kesi hiyo hadi Agosti 23 Mwaka huu.
Hata hivyo akiongea nje ya Mahakama Mshitakiwa SAED KUBENEA amesema kuwa utaratibu wa kisheria bado sio mzuri ni vyema kesi hiyo ingebaki polisi hadi hapo upepelezi utakapo kamilika na kwamba ni matumiI mabaya ya rasilimali za Serikali.
Aidha ameiomba Serikali iangalie mambo hayo Kwa kina kwani haina haja ya kukamata watu pale inapoona haina upelelezi wa kustosha.
Naye wakili anaemtetea mshitakiwa KUBENEA,ISAAC MWAIPOPO amesema kuwa wao bado wanasubiria upelelezi ukamilike kwani wana imani na Mahakama.
KUBENEA anakabiliwa na kesi ya shambulio kinyume cha Sheria kifungu namba 240 cha sheria ya makosa ya jinai sura ya 16 kilichofanyiwa marejeo mwaka 2002.
Mshitakiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo mnamo Juali 3 mwaka huu katika eneo la Bunge Mjini Dodoma.