November 25, 2024, 10:53 am
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KESI YA KABENDERA YAGONGA MWAMBA YASHINDWA KUENDELEA
Dar es salaam: Kesi inayomkabili Mwandishi wa Habari za Uchunguzi, nchini Tanzania Erick Kabendera, imesogezwa mbele hadi Novemba 20, 2019, baada ya Hakimu Augustine Rwizile, aliyekuwa akiisikiliza kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu, ambapo kwa sasa kesi hiyo inasubiri kupangiwa Hakimu mwingine.
Akizungumza mahakamani hapo leo Novemba 7, 2019, Wakili Mwandamizi wa Serikali Wankyo Simon, mbele ya Hakimu Mkazi Vicky Mwaikambo, amesema kuwa kesi hiyo ilifikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika.
Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu, likiwemo la utakatishaji wa fedha zaidi ya Shilingi milioni 173, uhujumu uchumi na ukwepaji wa kodi.
Kabendera alikamatwa nyumbani kwake Mbweni, Jijini Dar es Salaam, na watu waliodaiwa kuwa ni maafisa wa Polisi, Julai 29, 2019.