Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 12:56 am

NEWS: KESI YA HALIMA MEDEE HAKIMU MBIONI KUIPIGA CHINI SEREKALI

Dar es Salaam. Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam ameutaka upande wa mashtaka(Serekali) kuieleza mahakama kama hawana mashahidi katika kesi ya kutoa lugha chafu inayomkabili Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee dhidi ya Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli, ili wafunge ushahidi kwa kuwa shauri hilo lipo mahakamani hapo kwa miaka miwili sasa.

Tamko hilo la mahakama limekuja mara baada ya Wakili wa Serikali, Sylivia Mitando kudai leo Jumatatu Agosti 26,2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kuwa shahidi waliokuwa wanamtegemea kutoa ushahidi anaumwa.

"Leo nilijitahidi kuwasiliana na shahidi nilimpata lakini aliniambia hawezi kufika kwa sababu anaumwa hivyo naiomba mahakama hii ipange tarehe nyingine," amedai Mitando

Hakimu Simba amesema kesi hiyo ipo mahakamani hapo tangu Julai 10, 2017 hadi kufikia leo ni miaka miwili na mashahidi waliotoa ushahidi ni watatu hivyo naomba mfunge ushahidi kama wamemaliza.

Natoa nafasi nyingine ya mwisho leteni mashahidi waje kutoa ushahidi hadi sasa waliotoa ushahidi ni watatu tu sipendi ifike Oktoba mwaka huu nataka nilitolee uamuzi,” amesema Simba.

Shauri hilo limeahirishwa hadi Septemba 4, 2019 litakapokuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.

Inadaiwa kuwa Julai 3, 2017 katika ofisi za makao makuu ya Chadema zilizopo mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, Mdee alitamka maneno dhidi ya Rais John Magufuli kuwa, ‘anaongea hovyo, anatakiwa afungwe breki,’ kitendo kinachodaiwa kuwa ni kumdhalilisha Rais na kusababisha uvunjifu wa amani.