Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 10:33 am

NEWS: KESI YA ALIYEMUUWA MKEWE KWA KUMCHOMA NA MOTO MBIONI KUANZA

UPANDE wa mashtaka katika kesi ya mauaji inayomkabili mfanyabiashara, Khamis Luwonga maarufu kwa jina la Meshack (38), anayedaiwa kumuua mkewe Naomi Marijani kwa kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa, imeelezwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi wa kesi hiyo kuwa jarada la shauri hilo lipo kwenye hatua ya uchapaji.

Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon amedai hayo leo Novemba 18, mbele ya Hakimu Mkazi Salum Ally, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa

Wakili Wankyo amedai, shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi umekamilika na jarada lipo kwenye hatua ya uchapaji kwa ajili ya maandalizi ili lipelekwe Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) hivyo wanaomba tarehe nyingine ili waweze kufatilia suala hilo.

Hakimu Ally amearisha kesi hiyo hadi Desemba 2, mwaka huu .

Katika kesi hiyo ya muaji namba nne ya mwaka 2019, mshtakiwa Luwonga ambaye ni Mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam anadaiwa Mei 15, 2019 akiwa Gezaulole eneo la Kigamboni alimuua Naomi Marijani.

Inakumbukwa kuwa Hamis anadaiwa kumuua mke wake Naomi kisha kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya Mkaa ambapo alichukua majivu ya marehemu na kwenda kuyafukia shambani kwake