Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 11:40 pm

NEWS: KESI INAYOMKABILI RC MAKONDA YAANZWA KUSIKILIZWA LEO

Dar es salaam: Mashtaka 5 yaliyofunguliwa dhidi ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda likiwemo la kufoji vyeti vya elimu yataanzwa kusikilizwa leo.

Mashtaka hayo yaliyofunguliwa katika mahaka ya hakimu mkazi kisutu na Mayor wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob Tarehe 22 Mach 2017

Makonda anatuhumiwa kwa makosa matano ambayo ni Kughushi vyeti vya elimu yake, kujipatia mali kwa udanganyifu,kukiuka maadili ya Viongozi wa Umma, matumizi mabaya ya madaraka pamoja na kuvamia kituo cha radio Clouds fm.

Awali Meya Boniface aliwahi kuwakabidhi vielelezo vya ushahidi katikaTume ya maadili na Utumishi wa Umma na kwenye ofisi ya Kamishna kwa ajili ya hatua zingine ambazo wao wataona zinafaa.