- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KESI FREEMAN MBOWE NA VIONGOZI WA CHADEMA YAKWAMA
Kesi Na. 112/2018 ya uchochezi inayowakabili viongozi 8 wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA akiwemo Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe imepangiwa hakimu mwingine na imemfikia Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba na imepangwa kusikilizwa siku ya Alhamisi Tarehe 28 na 29 Machi 2019 ambapo upande wa mashtaka unatarajiwa kuleta mashahidi.
Kesi hiyo iliyokuwa ikitajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kelvin Mhina leo imepangwa rasmi kusikilizwa mbele ya Hakimu Simba baada ya hakimu aliyekuwa akiisikiliza kuanzia mwanzo, Wibard Mashauri kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ya uchochezi ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu na Naibu Katibu Mkuu Bara na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika.
Wengine ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.
Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwamo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari Mosi na 16, mwaka jana jijini Dar es Salaam.