Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 3:30 am

NEWS: KENYA KUANZA KUUZA MAFUTA ILIYOYAZALIASHA YENYEWE

Nchi ya Kenya sasa inakuwa nchi ya pili katika Afrika mashariki kuzalisha mafuta, imesema inaanza mchakato wa kuanza kuuza mafuta ghafi iliyokuwa inazalisha yenyewe katika Eneo la Turkana

Kenya iligundua mafuta mwaka 2012 katika mkoa wa Turkana, kaskazini mwa nchi hiyo, kwa kiwango kilichokadiriwa sawa na mapipa milioni 560.

Kenya ilianza kuzalisha mafuta mnamo mwezi Juni, na kuwa kwa mara ya kwanza nchi inayozalisha mafuta. Tangu wakati huo, Kenya inahifadhi bidhaa yake hiyo kwa kusubiri kuiuza na kuongeza kiwango

Tangu miezi minane iliyopita, malori yamekuwa yakisafirisha zaidi ya mapipa mia moja ya mafuta kwa siku kutoka Turkana.

Kufikia sasa, tayari Kenya imetoa mapipa 80,000 ambayo yanaendelea kuhifadhiwa kwenye matangi yaliyo mjini Lokichar

Related image

Kwa mujibu wa chanzo cha serikali, Kenya inatarajia kuongeza kiwango cha uzalishaji mnamo mwezi Mei, na hivyo kufikia mapipa 2,000 ambayo yatakuwa yakisafirishwa na malori. Visima vingine vya mafuta vitachimbwa na kufikia visma 300.

Hivi karibuni rais Uhuru Kenyatta alisema serikali yake imeweka mikakati ya kisheria, kuhakikisha kwamba wakati bidhaa hiyo itaanza kuuzwa, haitakuwa "laana" wala kuleta mvutano kama ulioshuhudiwa katika baadhi ya nchi zilizogundua mafuta katika siku za karibuni.