Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 3:35 am

NEWS: KAYA ZENYE VYOO BORA ZIMEONGEZEKA KUFIKIA ASILIMIA 62.4 NCHINI.

DODOMA: Kaya zenye vyoo bora nchini zimeongezeka hadi kufikia asilimia 62.4 mwaka 2019 kutoka asilimia 34 mwaka 2015 kupitia kampeni ya usichukulie poa, nyumba ni choo iliyoendeshwa kipindi cha miaka miwili na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto.


Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu katika kilele cha wiki ya usafi wa mazingira kitaifa na mkutano wa maafisa afya wa mikoa,halmashauri na wadau uliofanyika jijini hapa .


“Katika kipindi cha miaka miwili ya kampeni hii kaya zenye vyoo bora zimeongezeka ,vile vile kaya zisizokuwa na vyoo kabisa imepungua kutoka asilimia 7.5 hadi asilimia 1.9 katika kipindi hiki”Amesema Waziri Ummy.


Aidha, amesema kwa upande wa wa vijiji ambavyo kaya zake zote zina vyoo imeongezeka kutoka 743 hadi 4,311

kwa upande wa taasisi wameweza kuboresha huduma ya maji na usafi wa mazingira katika vituo vya tiba 1,267 kati ya lengo la vituo 1,000.


Hata hivyo amesema kuwa uchakuzi wa mazingira utokanao na taka ngumu umeendele kuwa changamoto katika maeneo ya mijini,hivyo serikali imejipanga kuongeza nguvu kwenye mamlaka za serikali za mitaa ili kuboresha miundombinu iliyopo katika mitaa hapa nchini.

“Serikali pia imeandaa mwongozo wa uwekezaji katika taka ngumu ili kuhamasisha uwekezaji na kuongeza jitihada za kuboresha usimamizi wa taka hapa nchini”.

Tafiti zinaonesha kwamba nchi inapoteza takribani asilimia moja ya pato ghafi la taifa(GDP) kutokana na hali duni ya usafi na utafiti uliofanywa na benki ya dunia mwaka 2012 ulionesha kwamba kila mwaka shilingi bilioni 450 zinapotea kutokana na madhara ya uchafu.