- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KAULI YA MBOWE BAADA YA LOWASSA KURUDI CCM
Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mh. Freeman Mbowe amewataka wanachama wa cha hicho kuwa madhubuti katika kipindi hichi cha mabadiliko katika chama
Mbowe ambaye pia ni mbunge wa Hai amesema kuwa kitendo cha wana CCM kuhamia Chadema kama chama kinabidi kitafakari kwa makini namna ya kuwapokea wanachama hao."Aidha, kurejea kwa Mhe. Lowassa CCM, kunatupa pia fursa ya kuzidi kutafakari kama chama hamia ya wana-CCM katika chama chetu nyakati za uchaguzi na maamuzi yetu na namna tunavyowapokea, hatuna budi kutulia na kumtakia maisha mema nyumbani alikorejea, sisi tuendelee na safari yetu yakuelekea Kigoma,"
katika ujumbe wake aliyeutoa jana March 2 kwa wanachama wa Chadema juu ya Edward Lowassa kurudi CCM amesema "wana-Chadema tunapotofakari jambo hili rejeeni kauli yangu ya wakati wote inayobeba falsafa yetu ya mabadiliko kwamba safari ya kusaka mabadiliko ni sawa na safari ya treni kutoka Dar es salaam kuelekea Kigoma, wapo wanaoanza na safari mwanzo wa safari na wapo wanaonzia katikati, pia wapo wanaoteremka njiani na wapo wanaoendelea na safari hadi mwisho, wote hao ni abiria, cha msingi kwetu hapa ni kuhakikisha safari yetu inaendelea, na ni imani yangu na matumaini yangu kwamba mtakubaliana na mimi kuwa safari yetu inaendelea." alisema Mbowe katika Ujumbe wake
Julai 2015, Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa alitangaza kuhamia Chadema na baadae kupitishwa na vikao vya chama kuwa mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbowe kwa sasa yupo gerezani Segerea baada ya kufutiwa dhamanana Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika kesi yao ya Uhaini inayowahusiha zaidi ya wanachama na viongozi 10 wa chama hicho.