- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KAULI 5 ZA MSEMAJI WA SEREKALI JUU YA CORONA
Msemaji mkuu wa Serekali Hassan Abbasi amewatahadharisha waaandishi wa habari nchini kuwa makini kwenye swala la Upashaji habari hasa kuhusu ugonjwa wa Corona nchini.
Dkt Abbasi ametoa kauli hiyo leo Aprili 11, 2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Dkt Abbasi amesema kuwa zipo habari nyingi za kupotosha kwenye mitandano ya kijamii juu ya Ugonjwa wa Corona, hivyo kuwataka wanahabari kuwa makini na Namna ya Kupasha watu habari.
1. “Mpaka sasa taarifa za kuzusha kuhusu COVID-19 zipo katika mitandao ya kijamii, niwakumbushe tu Sheria zetu zipo na zinafanya kazi, watanzania lazima tuhakikishe tunaisaidia jamii kuondokana na huu ugonjwa, tuache kusababisha taharuki”-Dkt. Hassan Abbasi, @msemajimkuuwaserikal
2. “Wakati tunaeleza ukweli kuhusu ugonjwa huu wa COVID-19 pia waandishi wa habari tueleze tatizo lilivyo na namna ya kuondokana na tatizo, Nchi yetu katika mapambano ya ugonjwa huu wa COVID-19 tumechukua hatua na tutaendelea kuchukua hatua kukabiliana nao”-Dkt. Hassan Abbasi
3. “Lazima vyombo vya habari vichukue tahadhari wakati huu tukiwa kwenye majukumu yetu ya kuhabarisha umma, Idara ya Habari-MAELEZO tumetoa muongozo kwa waandishi wa habari wa namna ya kutekeleza majukumu yao, tuutumie”-Dkt. Hassan Abbasi
4. “Tumeanza kutafakari namna tutakavyoendesha mikutano na waandishi wa habari, ikiwamo kutoa ‘Press Releases’, kurusha moja kwa moja na kusambaza ‘cleanfeed’ au kurekodi na kusambaza taarifa hiyo kwa waandishi wa habari,lengo ni kuepuka mikusanyiko”-Dkt.Hassan Abbasi