Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 9:21 pm

NEWS: KATIBU WA CCWT ALIA NA VIONGOZI.

DODOMA: Katibu mkuu wa chama cha wafugaji [CCWT]kata ya Bahi wilaya ya bahi mkoani Dodoma Dominic Bruno amewataka viongozi wa halmashauri ya bahi kuwa na ushirikiano na wafugaji ili kuleta maendeleo katika wilaya hiyo.

Akizungumza na muakilishi leo wilayani hapo amesema ili kuwa na maendeleo ni wajibu wa viongozi kuwa na ushirikiano ni pamoja nakukaa kujadili mambo mbalimbali katika harakati zakupambana na na maendeleo.

‘’suala la michango ni swalala hiali kwenye hii wilaya yetu mbaya zaidi wafugaji wamekuwa ni vitenga uchumi vya maeneo mengi mengi wanalazimishwa kulipakwa mfano sasa hivi kuna sheria inayoendelea kuwatafuana wafugajisharia ya mfuko wa elimu ambao ulianza kutumika mwaka 2014 kwa ajili ya kuwachangia wanafunzi wenye uhitaji’’ amesema.

‘’kutokana na sheria ya ndogo za ushuru za halmashauri ya wilaya zilizotungwa chini ya kifungu cha 7[1], [b] na [e] sura ya 290 ya sheria ya fedha za serikali za mitaa ni pamoja na kiwango cha tozo la vibali vya kupeleka mifugo mnadani kulipishwa Tshs. 4000’’ amesema Bruno.

‘’Mpaka sasa hatujui hizo hela zinatumika kufanyia nini nawamekusanya kiasi ganiwanafanya pasipo kushikishwa’’ amesema Brumo.

Akifafanua zaidi kuhusu suala hilo diwani wa kata ya bahi Agustino Ndono alisema ni kweli sheria ya wafugaji ya mfuko wa elimu wa kutozwa Tsh 2000 ipo na inaendelea kufanya kazi ile iliyokusudiwa

‘’ Uamuzi huu ulikubaliana na kikao cha waheshimiwa madiwani kilichoketi tarehe 29/07/ 2014 chenye muhtasariNa. BDC/ BM/06/07/2014 tozo hili Tshs. 2000 itaingia kama ushuru wa halmashauri na Tshs. 2000 ni kwajili ya mfuko wa elimuna hivyo hivyo Tshs. 1500 kwa mbuzi na kondoo.tozo la Tshs. 1000 itaingia kama ushuru wa halmashauri na tshs. 500 ni kwajili ya mfuko wa elimu.

‘’Kwa kila mfugaji atakapouza mfugo wake atachangia tshs 2000 kwa ajili ya mfuko wa elimu zile fedha zinapokusanywa zinapelekwakwenye mfumo wa elimu kwa matumizi ya kupeleka chakula katika mashule moja ya shule ni Mdemu ilipata msaada wa chakula mwaka jana.

‘’ sisi na mkurungezi wa bahi tumeamuwa hizi fedha kupeleka katika mabweni ya wanafunzi wakike ili kuwanunulia chakula kama unavyofahamu siku za nyuma bahi ili kuwa inaongoza kwa mimba za utoto tumefanya hivyo ili kupunguza matatizo madogomadogo’’ alisema Ndono.

‘’sisi tumekubaliana hizi fedha kupeleka katika shule zote za serikondali kwa ajili ya wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani yao wakiwemo wanafunzi wa kidato cha pili ili wasiwe wanarudi nyumbani mchana wakae shule wajisomee mpaka jioni’’ alisema Ndono.

Vilevile Ndono aliwaomba wananchi wa kata ya bahi kuwabana watoto wao na kuwasimamia pindi wanapokuwa shule ili kuweza kupambana na tatizo la watoto wa mitaani.

Sheria ya tozo la mfuko wa elimu ilianza kutumika tarehe 25/10/2015 ambapo pamoja na serikali kutangaza elimu bure lakini bado sheria hiyo inatumika mpaka sasa.