- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KATIBU MKUU WA UJENZI ATOA ONYO KALI KWA WAHANDISI
DODOMA: Katibu mkuu anayeshughulikia masuala ya ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga amewataka wahandisi nchini kuwa waadilifu katika utendaji wao wa kazi ili kujenga Tanzania ya viwanda.
Ameyasema hayo wakati akifunga mkutano wa maadhimisho ya siku ya wahandisi yaliyofanyika leo mjini Dodoma.
Katibu huyo amesema uzalendo katika shughuli mbalimbali utasaidia kujenga rasilimali za nchini na kuleta maendeleo katika jamii.
‘’ kuweni wabunifu kwa kutumia teknolojia inayoongeza ubora na inayopunguza gharama ‘’ amesema
Joseph Nyamhanga amezitaka taasisi mbalimbali kutumia vifungu vya sheria na kanuni ili kuwapa fursa mbalimabli wakandarasi
‘’Kumefunguliwa fursa kwaajili ya wakandarasi, kwa kazi ambayo haizidi billion 10 kwa ajili ya wakandarasi kutowapa wageni kama ni kazi za ndani zifanywe na wakandarasi wenyewe na billion 2 kwa ajili ya wahudumu wa ndani’’ amesema Nyamhanga.
Lengo la mkutano huo nikuwakutanisha wahandisi na wadau mbalimbali kujadili juu ya utendaji wao wa kazi.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni ‘’ mchango wa sayansi ,teknolojia ,uhandisi,na hisabati kwa ajili ya Tanzania ya viwanda.