- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KATIBU MKUU BAVICHA AJIVUA UWANACHAMA CHADEMA
Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema (BAVICHA) Edward Simbeye ametangaza kujivua uanachama wa Chama hicho, kwa kile alichokisema kutokuunga mkono baadhi ya mambo yanayoendelea ndani ya chama hicho kwasasa. Simbeye amesema kwa sasa anatafakari chama gani cha kujiunga nacho baada ya kujiondoa Chadema.
"Mambo ya Chadema yanatakiwa kuamuliwa kwa mujibu wa Katiba, Kanuni na miongozo ya chama, leo yanaamuliwa kwa kauli na amri za Mbowe, Mwenyekiti ameamua kugeuza chama kuwa mali yake binafsi, lakini tukitoka nje tunawaaminisha umma kuwa chama hichi ni mali ya Watanzania." Simbeye
Simbeye ametoa Msimamo huo Leo Februari 26, 20202 Jijini Dar es salaam, huku akisema kuwa Sera ya Sasa ya Chadema, Kila mtu ana haki ya kulinda utu wa mwenzie, "Je kumuita mwenzio mwanaume suruari, au panya hii Ni sawa?” alihoji
Simbeye amesema kuwa Chama cha Chadema kimepoteza Majiji mawili hivyo kilipaswa kujitafakari badala ya kuwaaminisha wananchi kuwa chama kiko imara
“Kuna mambo mengine kiungozi tunapaswa kuwa na akiba ya maneno kama ukiyasema, kuna leta mashara makubwa, tumepoteza majiji ya Dar es salaam na Arusha, bado tunawaambia Watanzania tupo imara, tunasema waende tu,” Simbeye
“Juzi nimeona tweet ya Mjumbe wa Kamati Kuu anasema wanaoenda ni Panya, kiongozi unaingia kwenye kiko kikubwa cha chama, unaamini anayeondoka ni Panya, Chama cha siasa ni watu.” Simbeye
Chadema hivi karibuni imekubwa na misukosuko ya Kisiasa juu ya swala la kuhama hama kwa viongozi na wanachama wake wakienda chama tawala CCM kwa madai ya kwenda kumuunga mkono Rais wa sasa wa nchi hiyo John Pombe Magufuli
Juzi tarehe 24 mwezi huu Madiwani kumi na moja kutoka chama hicho wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya walikihama chama hicho akiwemo meya wa jiji hilo, Kati ya madiwani hao, 10 ni wa kuchaguliwa kutokana kata mbalimbali na mmoja alikuwa wa viti maalumu ambao kwa pamoja wanasema wamekimbia magomvi katika chama chao cha awali.
Naye aliyekuwa katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Vicent Mashinji Februari 18 mwaka huu alitangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM). Mashinji alitangaza uamuzi huo katika ofisi ndogo za CCM, Lumunba jijini DSM na kupokelewa na Katibu Itikadi na Uenezi, Humprey Polepole