Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 3:31 am

News: Kassimu Tanzania inahistoria ya kuwa na watu wastaarabu na heshima.

Dodoma: Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa Majaliwa, amesema vyombo vya Ulinzi na Usalama vinaendelea kufuatilia matukio mbalimbali ya Uhalifu, ambayo yanatokea kwenye maeneo tofauti nchini na kuzua hofu kwa Wananchi.

Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuhakikisha wananchi wanaishi kwa Amani na Ulinzi ikiwemo wa Mali zao.

Ameyasema hayo wakati akijibu maswali kwenye kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu kutoka kwa Wabunge, ambapo amesema Serikali inafuatilia matukio yote ya Uhalifu kwa kufanya uchunguzi wa kina, ili kufahamu chanzo chake, na ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa wananchi watoe ushirikiano.

Tanzania ina historia ya watu kuwa na ustaarabu wa kuheshimiana, hivyo uchunguzi unaendelea kwa umakini, bila ya kuathiri upatikanaji wa taarifa muhimu.

Kuhusu kupotea kwa Mwanasiasa Ben Saanane kwa zaidi ya miezi sita, amesema vyombo vya ulinzi vya ndani vinaendelea kufuatilia suala hilo kwa umakini na uchunguzi ukikamilika taarifa itatolewa.

Waziri Mkuu alikua akijibu maswali kutoka kwa wabunge mbalimbali akiwemo kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe.