Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 5:46 pm

NEWS: KASILO: 'WAZAZI KAENI NA MABINTI ZENU KUWAEPUHA NA MIMBA ZA UTOTONI'.

DODOMA: Ikiwa siku chache kumalizika kwa mtihani ya darasa la saba kote nchini,wazazi wametakiwa kuwa karibu na watoto wao hasa mabinti na kuwaweka wazi juu ya mambo mbalimbali ili kuwaepusha na mimba za utotoni.

Akizungumza na muakilishi news mkurugenzi wa mtandao wa afya za wanawake Tanzania Gloria Kasilo alisema kuwa kipindi cha kusubiri matokeo ya darasa la saba ni kipindi kigumu kwa watoto wakike kwani wanaweza kuingia katika vishawishi na kupata mimba za utotoni.

‘’sisi tunashauri wazazi kuwa karibu na watoto hasa mabinti zetukatika kipindi hikiili kuwaeleza hali halisi ya maisha ni wakati gani unatakiwa kujiingiza katika mahusiano’’ alisema

Amesema moja ya makosa wanayofanya wazazi na kupelekea watoto wa kike kupata mimba za utotoni ni kutoweka ukaribu na watoto pamoja na kutowaweka wazi hali inayopelekea watoto kujifunza kupitia mitandao.

‘’Kwa sasa hivi wazazi wengi hatuna muda wa kukaa na watoto wetu tuko bize na kazi au biashara kwahiyohii inapelekea tunaamini watoto wetu wanatabia nzurikumbe wanatabia ambazo siyo nzuri wanajifunza kwenyemitando hata kwa marafiki zao’’ alisema.

Bi Gloria amewaomba wanaharakati na taasisi mbalimbali za kuwasaidia watoto wa kike kuzidi kutoa elimu ya afya ya jinsia hasa katika kipindi wanafunzi wanapomaliza mtihani wa darasa la saba ili kuwasaidia kushinda vishawishi.

‘’watu wenye nia njema na wadau wa afya wanaoweza kushauri wajitokeze kuona namna gani kuwashauri hawa mabinti zetu waweze kutulia majumbani wanapotoka wazazi kujua mtotoa anapotoka anaenda wapi na huko ndiko kunakotokea mimba za utotoni’’alisema Gloria.

Hata hivyo ameongeza kuwa wazazi kuwa mbali na watoto kunachangia kuongezea kwa mimba za utotoni katika jamii na kusahauri wazazi, wadau wa afya kutoa ushauri ili kusaidia kuwakinga na magonjwa watoto wa kike

Ikumbukwe kuwa moja ya changamoto inayowakabili watoto wakike wakati wakisubiri matokeo ya darasa la saba ni vishawishi ambavyo hupelekea kupata mimba za utotoni na kushindwa kujiunga na kidato cha kwanza.