Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 1:39 am

NEWS: KARDINALI WA KIKATOLIKI AKUTWA NA HATIA KWENYE KESI YA KINGONO

Mahakama ya Australia imemkuta na hatia ya kuwaingilia Kingono watoto 4 Wenye umri chini ya miaka 16 kiongozi wa hadhi ya juu wa Kanisa Katoliki Duniani, Kardinali George Pell wa Nchini Australia mwenye umri wa miaka 77.

Mashitaka yalifunguliwa tangu Desemba 11 mwaka jana, lakini vyombo vya habari vilikuwa vimepigwa marufuku kutoa taarifa hiyo baada ya kutahadharishwa kufunguliwa mashitaka. Lakini pamoja na kuondolewa kwa marufuku hiyo, Jumanne wiki hii, taarifa hiyo imetangazwa kwenye vyombo vya habari.

Kardinali George Pel amekutwa na hatia, ikiwemo ya kumuingilia mtoto wa umri ulio chini ya miaka 16, na hatia zingine nne za kuwafanyia vitendo visivyo vya kawaida watoto wa chini ya miaka 16.

Hata hivyo Kardina Pell amekanusha tuhuma hizo dhidi yake .

Pell mwenye umri wa miaka 77 anatarijiwa kuhukumiwa siku ya Jumatano, lakini mawakili wake wanasema kua watakata rufaa hatia hiyo.

Kardinal George Pell ambaye ni kiongozi wa kanisa aliyekuwa anashikilia nafasi ya Muweka hazina, ni miongoni mwa viongozi wenye nguvu zaidi kanisani.

Kanisa Katoliki duniani kote kwa miaka ya hivi karibuni, limeendelea kukumbwa na kashfa ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto, na kudaiwa kuwa wamekua wakificha masuala hayo.