- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KANISA LA KKKT LATAJA MAMBO 4 MAZITO 2019 IKIWEMO UCHAGUZI SEREKALI ZA MITAA
Moshi. Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), wametoa salamu za Krismasi na mwaka mpya, huku mkuu wa kanisa hilo, Askofu Fredrick Shoo akijikita katika imani, elimu na siasa hususani uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Novemba 24, 2019
Sambamba na hilo pia katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) na viongozi wa baadhi ya mikoa nao wametoa ujumbe wao wa mwaka mpya.
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dk Stephen Munga alienda mbali na kuielezea Noeli au Krismasi kuwa ni jibu kwa wenye nguvu na mamlaka wanaodhani dunia na vyote vilivyomo ni mali yao.
Salamu hizo zitasomwa rasmi keshokutwa Jumatano katika Dayosisi za makanisa hayo.
Katika salamu zake kwa waumini wa KKKT nchini, Askofu Shoo alisema mwaka 2019 uliobakiza siku tisa kumalizika haukuwa mteremko na raha bali ulikuwa na changamoto nyingi za kimaisha.
“Tumeshuhudia baraka nyingi za Mungu kwetu, lakini pia magumu na changamoto nyingi za kimaisha. Wapo waliouguliwa sana na hata kuondokewa na wapendwa wao,” alisema Askofu Shoo.
“Wengine wamepata wakati mgumu hata jinsi ya kulipa gharama za elimu za watoto wao pamoja na kuwapatia mahitaji mengine muhimu kutokana na changamoto za kiuchumi,” alisisitiza Dk Shoo.
“Mwaka huu pia tumeona uchaguzi wa serikali za mitaa ukifanyika. Kama kawaida ilivyo kwa nchi za Afrika, uchaguzi huu haukupita bila kuwapo kwa changamoto,” alisema.
“Tumeshuhudia sintofahamu kadhaa katika mchakato mzima jambo lililosababisha tukaingia katika uchaguzi bila kuwa na muafaka wa pamoja wa wadau mbalimbali muhimu vikiwamo vyama vya siasa,” aliongeza Askofu Shoo.