Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 5:01 pm

NEWS: KANISA KATOLIKI LAWAMANI KWA KUPORA SHAMBA LA KIJIJI

DODOMA: Baadhi ya wakazi wa kijiji Cha mpunguzi kata ya Mpunguzi katika manispaa ya Dododma wameingia katika mgororo wa shamba na kanisa katoliki jimbo la Dododma mjini.

Wanadai kuwa mgogoro kati yao na jimbo katoliki umekuja mara baada ya kanisa hilo kuomba kupewa eneo hilo lenye ukuwa wa hekari mia mbili kwa madai kuwa watajenga huduma za kijamii ikiwemo miundombinu ya maji na barabara pamoja kituo cha vijana.

hiyo ni baadhi ya nyumba ambazo zilimbomolewa

“Ilikuwa mwaka 2006 ambapo jimbo walisema tutoe eneo hili kwa ajili ya kutuletea maendeleo, na sisi tulikubali kwa moyo mmoja kwa kuwa maendeleo tunayapenda, lakini cha kushangaza kuanzia muda huo hadi sasa hakuna kilichofanyika” Alisema Juma Mselia aliyevunjiwa nyumba yake

Alisema baada ya kuona hakuna chochote kilichofanyika toka watoe eneo hilo walikuwa hawapewi ushirikiano kutoka kwa viongozi wao wa kijiji na ndipo walipowataka viongozi wao wauvunje mkataba waliongia na kanisa hilo ili waendelee kumiliki maeneo yao.

“Baada ya kuona ni zaidi ya miaka kumi sasa tangu tutoe eneo lakini hakuna kilichofanyika, tukaamua kuwaambia viongozi wetu kuwa tunataka tukae meza moja na kanisa ili tuvunje mkataba, lakini kiongozi wetu hakutaka kuonyesha ushirikiano” Alisema Lilian Funika.

huyo ni miongoni mwa mama ambaye nyumba yake ilibomolewa

Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa kijiji hicho ambapo wakati wa utawala wake ndipo yalifanyika makubaliano hayo Alfa Zakayo alisema kuwa eneo hilo sio la mwananchi mmoja mmoja bali ni eneo la kijiji hivyo wananchi wameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuona ahadi zilizotolewa na jimbo kama makubaliano hazitatekelezwa.

“Ni kweli eneo hilo lilichukuliwa mikononi mwangu kwa ahadi kuwa watachimba visima vya maji, watajenga kituo cha vijana kwa ajili ya kutoa elimu pamoja na makazi ya Askofu, lakini baadaye ofisi ya jimbo ilituletea barua kuwa wameshindwa kuendeleza hili eneo kwa sababu ya vikwazo ndani ya viongozi wa kijiji, hivyo kijiji kina haki ya kuchukua eneo lake” Alisema Zakayo.

huyo ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa kijiji kwa mwaka huo

Uongozi wa jimbo katoliki umeshindwa kutoa ushiriano kwa mwandishi wa habari na kuanza kutupiana mpira kwani katibu wa kanisa hilo alisema yeye sio msemaji wa jimbo na kutoa namba ya mwanasheria wao kwa madai kuwa ndio msemaji, ambaye naye alisema siyo msemaji na kusema kuwa katibu ndiye anayejua msemaji wa jimbo.