- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KANISA KATOLIKI LAPENDEKEZA WANAUME WALIO OA KUWA MAKASISI
Kanisa Katoliki limekuja na wazo la kuwaruhusu wanaume waliooa kuwa makasisi hasa katika maeneo yanayozunguka mto Amazon, katika bara la Amerika Kusini.
Maeneo hayo ambayo ni mbali, na yapo katikati ya msitu mnene, yana uhaba mkubwa wa makasisi, na bara la Amerika Kusini lina wafuasi wengi wa Ukatoliki.
Iwapo suala hilo litapitishwa, itakuwa ni mabadiliko makubwa ndani ya kanisa hilo kwa kipindi cha miaka 1000.
Mabadiliko hayo yamependekezwa kwenye Waraka muhimu wa Mazingira wa Papa - Laudato Si - uliochapishwa mwaka 2015.
Katika waraka huo, Papa Francis, ambaye ndiye kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki ameandika kuwa, eneo hilo la Amazon linakabiliana na na changamoto ambazo (kuzitatua) "inahitaji mabadiliko ya kimfumo na kibinafsi kwa watu wote, mataifa yote (ya eneo hilo la Amazon) pamoja na Kanisa."
Eneo hilo lina wakazi takribani milioni 33 na ni chanzo muhimu cha maji safi (moja ya tano ya dunia), hewa safi ya oksijeni (moja ya tano ya dunia) na moja ya tatu ya hifadhi ya misitu duniani.
Vatican inasema eneo hilo hata hivyo linaibua changamoto kubwa ya kikasisi na kimazingira - lakini ni uhaba wa makasisi ambao Kanisa linaweza kupata ufumbuzi wake wa moja kwa moja.