- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KANGI LUGOLA AHOJIWA NA TAKUKURU KWA SAA 6
ALiyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi wa Tanzania na MBUNGE wa Jimbo la Mwibara Kangi Lugola leo amefika katika Ofisi za TAKUKURU mjini Dodoma kwaajili ya mahojiano.
Lugola amefika Katika ofisi hiyo mapema asubuhi na kuhojiwa kwa zaidi ya saa 6.
Kangi ambaye alitenguliwa uteuzi wake kwa tuhuma za kushiriki kuingia mkataba wa trilioni moja wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na kampuni ya kigeni kutoka Romania alifika Makao Makuu ya Ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuhojiwa majira ya Saa moja asubuhi.
Mkononi akiwa ameshikilia Ilani ya Chama cha Mapinduzi na Mkoba ulio na nyaraka alitembea kwa kujiamini kuingia katika Ofisi hizo zilizopo eneo la Jamhuri mjini Dodoma.
Mbali na Kangi wengine ambao anatuhumiwa nao ni pamoja na aliyekuwa Kamishna Jeneral wa Zimamoto na uokoaji, Thobias Andengenye, Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jacob Kingu na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Yusuph Masauni wote watahojiwa leo kwa nyakati tofauti.
Thobias Andengenye, ataingia kuhojiwa majira ya 9:30 asubuhi, Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jacob Kingu ataingia kuhojiwa majira ya 2:00, mchana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Yusuph Masauni ataingia kuhojiwa majira ya saa 6.00 jioni.