- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KAMPUNI ZA SIMU ZAINGIA MATATANI
DAR ES SALAAM: MAMLAKA ya Mawasilianio Tanzania (TCRA) imeamuru kampuni zote za simu za mkononi zinazofanya kazi nchini, kusitisha mara moja kutoa matangazo kwenye huduma za mawasiliano kwani ni kinyume cha Kanuni za Huduma za Ziada na Kinga ya Mlaji za Mwaka 2015 na 2011, na atakayekaidi atafutiwa leseni.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba alitoa agizo hilo jana Dar es Salaam baada ya kukutana na wawakilishi wa kampuni za simu za mkononi kutokana na kuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa watumiaji wa huduma, zinazotolewa na kampuni hizo juu ya matangazo hayo, yanatolewa kabla ya mpigaji simu kuunganishwa.
Kilaba alisema hatua ya zuio la matangazo hayo kabla ya simu ya mteja kuunganishwa, linatokana na mamlaka hiyo kujiridhisha kuwa watoa huduma wengi wa mawasiliano ya simu za mkononi nchini, wamekuwa wakikiuka vigezo na masharti kama yanavyoelekezwa katika kanuni za huduma za ziada.
Hivyo, mamlaka imezuia kampuni hizo kusitisha mara moja utoaji wa matangazo hayo kuanzia jana Julai 6, 2017 ili kuondoa kero. Mtoa huduma yeyote ambaye atakiuka agizo hilo, atakabiliwa na adhabu kadhaa ikiwemo kufutiwa leseni ya kuendesha biashara ya utoaji wa huduma za mawasiliano nchini.
source: habarileo