- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KAMPUNI YA BARRICK YATANGAZA KUPUNGUZA WAFANYAKAZI
Kampuni ya kuchimba Madini nchini Tanzania ya Barrick Mining imetangaza kupunguza idadi ya wafanyakazi katika Mgodi wa North Mara ili kumudu gharama za uendeshaji wa Kampuni hiyo kwa sasa.
Kwa mujibu ya taarifa iliyotumwa kwa wafanyakazi Januari 13, uamuzi huo unatokana na tathmini iliyofanywa kubaini kama mgodi huo una wafanyakazi wenye taaluma zinazohitajika wakitekeleza majukumu yanayowahusu ama la.
“Kwa kuzingatia sheria ya nchi tunawajulisha wafanyakazi wote, na nakala tukiwa tumeipeleka Numet (Chama cha Wafanyakazi Mgodi wa North Mara) kuhusu dhamira hiyo,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa na meneja wa mgodi huo, Luiz Correia.
Mgodi huo uliokuwa unamilikiwa na Acacia hivi sasa upo chini ya kampuni ya Twiga iliyoundwa kwa ubia wa Serikali na Barrick Gold Corporation iliyokuwa kampuni mama ya Acacia.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, upunguzaji huo utawahusu wafanyakazi 110 kutoka idara ya rasilimaliwatu, uchimbaji, usimamizi wa mali pamoja na ugavi.
Wengine watakaoathirika ni kutoka idara ya uhandisi mitambo, huduma kwa jamii, mazingira na usalama kazini.
Meneja wa mgodi huo, Correia alisema pazia la mawasiliano kati ya uongozi na chama cha wafanyakazi limefunguliwa wakati wafanyakazi wakisubiri matokeo ya uamuzi utakaoafikiwa na pande hizo mbili.
Numet kinasimamia masilahi ya waajiriwa mgodini hapo.