- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KAMBI RASMI YA UPINZANI WASHTUKIA UBOVU WA VITABU SHULE ZA MSINGI
DODOMA: Kambi rasmi bungeni jana imeitaka serikali kufuta mara moja vitabu vyote ambavyo vimepelekwa katika shule za msingi huku vikiwa na makosa mengi.
Mbali na hilo walisema hatua kali zichukuliwe kwa kitendo cha kupitisha vitabu hivyo wakati ikifahamika wazi kuwa havina kiwango.
Akiwasilisha maoni ya kambi rasmi ya upinzani bungeni,Suzan Lyomo wakati wa kuwasilisha maoni ya bajeti ya Wizara ya Elimi,Sayans,Tknolojia na ufundi , alisema kitendo cha kupitisha vitabu hivyo ni kulisababishia taifa hasara kubwa na kushusha kiwango cha elimu nchini.
Mbali na hilo kambi rasm ya upinzani bungeni ilitaka serikali ieleze imepata wapi fedha za ujenzi wa mabweni ya chuo kikuu cha Dar es Salaam kwani bunge ambalo hupitisha bajeti ya matumizi hakuna mahali popote walikopitisha fedha hizo.
Hata hivyo serikali imesema imebaini uwepo wa baadhi ya vitabu vyenye makosa ya kimaudhui.
Akizungumza wakati wa kuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojoa na Ufundi kwa mwaka wa fedha 2017/2018, Waziri Prof.Joyce Ndalichako, alisema licha ya kubaini vitabu hivyo, uchambuzi wa kina unafanyika kwa vitabu vyote vilivyochapishwa mwaka 2016/2017.
Ndalichako alisema uchambuzi huo una lengo la kubaini endapo dosari zilizobainika katika baadhi ya vitabu haijajitokeza kwenye vitabu vingine.
Alisema mchakato wa kuchukua hatua za kinidhamu kwa mujibu wa taratibu za utumishi umekwishaanza kwa watumishi ambaovitabu walivyoidhinisha kuwa viko sahihi vimebainika kuwa na makosa.
“Napenda kulihakikishia bunge kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wahusika ili kukomesha tabia ya uzembe kwenye kazi muhimu za taifa,” alisema Prof.Ndalichako.
Vilevile, alisema baada ya uchambuzi kukamilika kwa vitabu vyote vilivyochapishwa wizara itafanya maamuzi kuhusu hatua za kuchukua dhidi ya vitabu ambavyo vitabainika kuwa na dosari.
Akizungumzia makosayaliyopo kwenyevitabu, waziri kivuli wa kambi rasmi ya upinzani, Susan Lyimo, alisema vitabu vina makosa mengi ya lugha ya Kiswahili na Kiingereza.
Susan alisema kutokana na makosa na mapungufu yaliyopo kwenye vitabu hivyo, serikali inatakiwa kuzuia matumizi yake mashuleni.
Alisema serikali pia inatakiwa kuiagiza taasisi ya Elimu kufanya marekebisho ya makosa yaliyopo kwenye vitabu hivyo na kuvichapisha upya na kuitaka serikali kufanya uhakiki wa taaluma na weledi wa watumishi wa Taasisi ya Elimu Tanzania ili kujiridhisha kama wana sifa stahiki, uwezo na weledi katika kufanya kazi ya utunzi wa vitabu.
Aliongeza kwa kusema wameamua kupendekeza hivyo kwa kuwa serikali inapata hasara kubwa kurudia kuchapisha vitabu hivyo kutokana na uzembe wa watumishi wanaohusika na kazi hiyo au watumishi wasio na utaalamu katika kazi wanayoifanya.
WAHADHIRI KUSOMESHWA
Katika mwaka wa fedha 2017/2018,Ndalichako alisema wizara yake itasomesha wahadhiri 100 katika Shahada ya Uzamivu kwenye fani zilizo na uhaba mkubwa wa wahadhiri katika vyuo vikuu vya umma.
Ndalichako alisema hatua hiyo itawezesha kuhakikisha elimu inayotolewa nchini ina ubora unaotakiwa huku ikijenga shule ya kisasa ya sekondari katika mkoa wa Dodoma kwa lengo la kuongeza miundombinu ya elimu katika makao makuu ya nchi.
Aidha, alisema katika mwaka wa fedha 2017/2018 wizara yake itatekeleza ongezeko la idadi ya wanafunzi wa shahada za awali kutoka 24,182 hadi 25,900 ongezeko ambalo ni asilimia saba na wanafunzi wa shahada na stashahada za uzamili kutoka 2,092 hadi 2,510.
Alisema wanafunzi wa stashahada na astashahada wataongezeka kutoka 182hadi 218 ongezeko ambalo ni la asilimia 20.
UJENZI, UKARABATI WA VYUO,SHULE
Waziri huyo alisema katika mwaka huu wa fedha serikali itaendelea na ujenzi na ukarabati wa vyuo sita vya ualimu vya Kleruu, Mpwapwa, Dakawa, Tabora, Butimba na Marangu.
Vilevile, alisema itafanya ukarabati wa miundombinu ya ya maktaba na maabara za TEHAMA katika vyuo vya ualimu 35 ili kuweka mazingira rafiki ya kujisomea kwa wanafunzi na wanachuo. Vyumba vya madarasa 2,000 kwa shule za msingi na sekondari.
Waziri alisema kupitia program ya Lipa Kulingana na Matokeo, wizara yake itaendelea kuratibu ujenzi wa
Madarasa 2,000 kwa shule za msingi na sekondari na kukarabati wa shule kongwe 17 ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa madarasa na kuwafanya wanafunzi kujifunza kwa ufanisi mkubwa.
Alisema wizara yake itagharamia ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya maji na vyoo katika shule za msingi 1000 na sekondari 200 kwenye mikoa ya Dodoma, Mara, Tabora, Mwanza, Kagera, Kigoma, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Simiyu na Shinyanga.
MIKOPO ELIMU YA JUU
Akizungumzia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), mwaka wa fedha uliopita, Ndalichako alisema serikali ilitoa mikopo kwa wanafunzi 122, 374 ambapo wanafunzi 28,785 ni wapya ambao mkopo wao unagharimu sh. bilioni 104.6 na wanafunzi 93,559 ni wale wanaondelea na masomo ambao unagharimu sh. bilioni 379.2
Alisema bodi hiyo ilitoa ruzuku ya sh. bilioni 4.6 kwa ajili ya wanafunzi 1,584 wanaoendelea na masomo ndani ya nchi na sh. Milioni 811.09 kwa wanataaluma 44 wanaondelea na mafunzo ya uzamivu nchini Ujerumani.