- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE VIWANDA,BIASHARA NA MAZINGIRA YASHAURI BIDHAA ZA NJE ZIONGEZEWE KODI.
DODOMA: Serikali imeshauriwa kuona namna ya kuongeza kodi kwa bidhaa zinazotoka Nje ya Nchi ili ziende sawa na zile zinazozalishwa hapa nchini lengo ni kulinda bidhaa zinazozalishwa hapa nchini nazo kupata soko.
Ushauri huo umetolewa Jijini Dodoma na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara na Mazingira, Kanali Mstaafu,Masoud Ali Khamis wakati akizungumza katika semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRAD).
Khamis ambaye ni Mbunge wa Mfenesini (CCM) amedai kwamba viwanda vya ndani vimekuwa vikikabiliwa na changamoto ya bei katika soko kuwa kubwa kuliko bidhaa zinazotoka nje ya Nchi hivyo ameishauri Serikali kuangalia namna ya kuongeza kodi kwa bidhaa zinazotoka Nje ya Nchi ili ziendane na bidhaa za ndani.
“Lakini itafutwe mbinu ya kufanywa hapa ili wenzetu wa viwanda vya ndani wauze bidhaa zao tatizo letu kubwa la viwanda vya Tanzania ni bidhaa zetu kuwa zina bei ya juu na ‘Production Cost’ ya viwanda vyetu ipo juu kuna umeme na mambo mengine mengi," amesema Khamis.
Ameongeza kuwa “Kwa sababu wangetumia matumizi ya chini sasa hivi kiwanda kinaweza kuzalisha mali zikajaa kwenye magodauni wafanyakazi bado anao hawafanyi kazi lakini anawalipa mishahara na hili ni tatizo"amesema.
Kuhusu changamoto ya baadhi ya viwanda kukosa masoko,Makamu Mwenyekiti huyo amesema jambo hilo sio mara ya kwanza kulifikisha Serikalini ambapo amesema kwamba linahitaji kuangaliwa kwa umakini.
Kwa upande wake,Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE)Edwin Rutegaruka amesema wameweka mikakati endelevu ya kuzalisha bidhaa kulingana na mahitaji ya soko.
Pia,amebainisha kuwa wameangalia namna gani ya kuwaunganisha wazalishaji ili waweze kuzalisha bidhaa zinazohitajika sokoni kwa kuanzisha vikundi ambavyo vitawapa majibu kujua mahitaji ni yapi katika soko ili waweze kufanya biashara zao kwa urahisi.
“Pia tuna Intelejensia ya masoko, tumeweka mpango mkakati wa kuyaelewa masoko yanataka nini tunatarajia 2020 tuweke mifumo mizuri na kwa kuanzia tayari tuna Maafisa Masoko 35 kwa ajili ya kujua soko linataka nini na tutaanza na masoko ya jirani yanataka nini na baadae tutaenda katika masoko makubwa yanataka nini" amesema.