- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Kamanda Sirro hatua kali zitachukuliwa kwa yoyote atakaye jichukulia sheria mkononi
Dar es salaam: Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Simon Sirro amewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi badala yake waviachie vyombo husika ili viweze kufanya kazi yake.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Sirro Amesema kuwa wananchi kujichukulia sheria mikononi pindi wakamatapo watuhumiwa ni kinyume cha sheria hivyo wanatakiwa kuacha mara moja tabia hiyo.
“Ni vyema wananchi wakaacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi ili vyombo usika vifanye kazi yake,”amesema Sirro.
pamoja hayo amesema kuwa wananchi kuwauwa watuhumiwa ni kosa kisheria kwani watakao bainika kufanya hivyo sheria kali dhidi yao zitachukuliwa.
Hata hivyo, ameongeza kuwa ni bora wananchi waache tabia hiyo ya kujichukulia sheria mikononi kwani vyombo husika kama Polisi na Mahakama vipo kwa ajili ya shughuli hiyo