Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 10:53 am

NEWS: KAIMU JAJI MKUU AWAONYA WANASHERIA WATAKAO GOMA KUFANYA KAZI

Dar es salaam: Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma amesema atawachukulia hatua za kinidhamu Mawakaili watakaoshiriki mgomo wa kufanya shughuli za mahakama uliotangazwa na chama cha mawakili TLS kupitia Rais wa chama hicho, mbunge Tundu Lissu.

Prof. Juma ameyasema hayo leo baada ya Rais wa Chama cha mawakili Tanzania Tundu Lissu Tarehe 27 Agosti mwaka huu kutangaza kuwepo kwa mgomo kwa mawakili wote nchi Nzima kushinikiza serekali kufanya uchunguzi wa tukio la Kulipuliwa kwa Ofisi ya IMMMA Advocates zilizopo Upanga Jiji Dar es salaam.