- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KABUDI: 'HALI YA USAJILI NA TAKWIMU ZA NDOA NI MBAYA'
DODOMA: HALI ya usajili na takwimu za matukio ya vizazi,vifo ndoa na talaka nchini hairidhishi kutokana na takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 zinaonyesha kuwa asilimia 13.4 ndio wamesajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa.
Kauli hiyo imetolewa leo Mjini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria,Profesa PALAMAGAMBA KABUDI wakati alipokuwa akifungua kikao cha wadau kuhusu usanifu mpango wa usajili wa matukio muhimu ya binadamu na ukusanyaji wa takwimu.
Profes KABUDI amesema kuwa kufuatia kuwepo kwa hali hiyo Serikali imeamua kufanya maboresho ya Mfumo wa usajili wa matukio muhimu ya binadamu kwa lengo la kutatua changamoto mbalimbali kutokana na hali ya usajili nchini kutokuwa ya kuridhisha.
Aidha amebainisha kuwa Idadi hiyo ni ndogo na ni kiashiria kuwa Serikali haina taarifa za idadi kubwa ya wananchi ambapo licha ya kuwepo kwa takwimu hizo hivyo kukosa kumbukumbu.
Pia Profesa KABUDI amesema kuwa maboresho hayo yanatekelezwa kupitia mkakati wa Kitaifa wa usajili wa matukio muhimu ya binadamu na kwamba usajili wa matukio muhimu ndio mfumo mama katika nchi yoyote.
Kwa upande wake Profesa HAMISI DIHENGA ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya wakala wa Usajili,udhamini na ufilisi (RITA)amewataka wananchi wote kujitokeza kwaajili ya kujisali ili wapate vyeti vya kuzaliwa.
Hata hivyo Profesa Dihenga amesema kuwa wananchi wengi wamekuwa hawana elimu juu ya usajili jambo ambalo limepelekea waliojisajili kuwa wachache.