Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 3:38 am

NEWS: KABILA AKUTANA NA MUUNGANO WA CHAMA CHAKE

Rais mstaafu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila amekutana Jumatano wiki hii na wawakilishi wa muungano wa vyama tawala chini ya utawala wake, FCC, katika shamba lake la Kingakati jijini Kinhsasa.

Katika mkutano huo Bw Kabila amewapa mwelekeo mpya wa chama hicho baada ya aliyekuwa mgombea kwa tiketi ya FCC Emmanuel Ramazani Shadary kushindwa kupata kiti cha urais katuika uchaguzi wa desemba 30 mwka uliopita.

Akizungumza wakati wa mkutano huo mratibu wa FCC Nehemie Mwilanya, amewaambia wasimamizi wa vyama hivyo kuwa mpango mpya uliopo, ni kukubali kubaki waaminifu kwa rais Joseph Kabila, na kuheshimu maelekezo yote ya FCC.

Katika hatua nyingine mratibu huyo pia amesema lengo kuu kwa sasa ni kumuandalia Jospeh Kabila mazingira ya kuchaguliwa tena kuwa rais wa nchi hiyo, katika uchaguzi utaoandaliwa baada ya muhula huu wa miaka mitano,

Taarifa kutoka makao makuu ya chama hicho cha FCC imesema Ijumaa Februari 22, Kabila atakutana na wabunge wote wa muungano huo wa FCC waliochaguliwa, na ambao ndio wengi katika bunge la taifa nchini DRC.