Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 2:50 am

NEWS: KABENDERA AWALIZA NDUGU ZAKE MAHAKAMANI LEO.

Dar es Salaam. Kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Mwanahabari wa Habari za Uchunguzi Erick Kabendera imeendelea tena hii Leo Januari 2, 2020 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam Wakati upande mashitaka ukieleza Mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Sababu ya ndugu na Kabendera kulia ni inatokana na mshatakiwa huyo kufiwa na mama yake mzazi, Verdiana Mujwahuzi Jumanne ya Januari 31, 2019 katika Hospitali ya Rufaa Amana, Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Mwili wa Verdiana (80) utaagwa kesho Ijumaa katika Kanisa Katoliki Chang’ombe, Temeke jijini Dar es Salaam kisha utasafirishwa kwenda Bukoba mkoani Kagera kwa maziko yatakayofanyika Januari 6, 2020.