Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 2:52 am

NEWS: KABENDERA AACHA UJUMBE MZITO ATAKA WANANCHI KUMUOMBEA

Mwandishi wa habari nchini Tanzania, Erick Kabendera amewashukuru Watanzania kwa kuuungana na familia yake kuomboleza kifo cha mama yake mzazi Verdiana Mjwahuzi (80).

Verdiana aliyefariki dunia Jumanne iliyopita ya Desemba 31, 2019 katika Hospitali ya Rufaa ya Amana jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa siku mbili kwa matibabu zaidi.

Leo Ijumaa Januari 2, 2020 kulifanyika Ibada ya kuuaga mwili wa Verdiana katika Kanisa Katoliki la Mt. Francis Xavier Chang'ombe, Temeke, Dar es Salaam ambapo mamia ya waombolezaji kutoka ndani na nje ya Tanzania wamejitokeza.

Jana Alhamisi, maombi ya Kabendera ya kuhudhuria ibada hiyo ya kuaga mwili wa mama yake yaligonga mwamba baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuyatupilia mbali ikisema haina mamlaka hayo na hayawezi kukatiwa rufaa.

Baada ya uamuzi huo, Kabendera alirejeshwe gereza la Segerea anakokaa tangu Agosti 5, 2019 kutokana na mashtaka matatu anayokabiliwa nayo ikiwamo la uhujumu uchumi na utakatishaji fedha zaidi ya Sh173 milioni.

Erick amejaribu kuandika ujumbe kwenu ambao alitaka niusome mbele yenu Mbunge Zitto Kabwe ameongea

Amepata taabu sana kuandika na kufuta ili kufikisha ujumbe anaoutaka. Ameniambia ametumia na karibu kurasa 20 kuandika ujumbe huu usiku mzima wa jana. Anaandika na kufuta.


Uchungu wa kuondokewa na mama ni mkubwa sana, hasa anapokuwa ameondoka na umeshindwa kumuaga kama ilivyotokea kwangu.

Hata hivyo nimefarijjka kwa Watanzania wote walioguswa na msiba huu bila kujali itikadi zao za kisiasa na kidini na kunisaidia kumsitiri Mama yangu.

Upendo huu umeonyesha nchi ambayo nimeipenda na naipenda kutoka moyoni. Shukrani za dhati ziwafikie watu wote kwa upendo wao na ushiriki wao kufanikisha msiba wa Mama yangu.

Mwenyezi Mungu na awabariki sana na kuwaongezea pale mlipopunguza kwa ajili yangu.

Mtuombee.

"Uchungu wa kuondokewa na mama ni mkubwa sana, hasa anapokuwa ameondoka na umeshindwa kumuaga kama ilivyotokea kwangu."

"Hata hivyo, nimefarijika kwa Watanzania wote walioguswa na msiba huu bila kujali itikadi zao za kisiasa na kidini na kunisaidia kumsitiri mama yangu," amesema Zitto ambaye pia ni Kiongozi wa ACT-Wazalendo

Amesema upendo huo umeonyesha nchi ambayo ameipenda kutoka moyoni.

"Shukrani za dhati ziwafikie watu wote kwa upendo wao na ushiriki wao kufanikisha msiba wa mama yangu. Mwenyezi Mungu na awabariki sana na kuwaongezea pale mlipopunguza kwa ajili yangu. Mtuombee," amesema Zitto katika salamu hizo