"Kusudio la kufanya maandamano ya amani nchi nzima limetolewa na mkutano mkuu, mkutano ulituagiza kufanya maandamano ili kuongeza hamasa, ili kuweza kurejesha mchakato wa katiba, tumemuomba Rais apokee haya maandamano kwa sababu ya mambo mawili, la kwanza ni kumpongeza kwa kazi nzuri anayoifanya, la pili ni kufikisha ujumbe wetu wa katiba, kwamba aturudishe kwenye mchakato", amesema Mwakagenda.
Mwakagenda ameendelea kwa kuomba na kulitaka Jeshi la Polisi kuwapa ulinzi wa kutosha siku hiyo, kwani wanalotarajia kulifanya ni suala la kisheria na lenye uzalendo, kwa ajili ya wananchi wa Tanzania, na kuwataka wananchi kushiriki kwenye maandamano hayo, ili kuunga mkono juhudi zao za kutaka kurudishwa kwa mchakato wa katiba na kupata muafaka wake.