Tukio hili limetokea, mapema leo siku ya Jumatatu kwa mujibu wa Televisheni ya nchi hiyo Al Hadath.
Aidha, inaelezwa kuwa, pamoja na Waziri Mkuu Hamdok, maafisa wengine wa serikali ya mpito akiwemo Waziri wa Ulinnzi na Mawasiliano pia wamekamatwa.
Hii inakuja, kufuatia nchi hiyo kuendelea kushuhudiwa maandamano kati ya wanaoiunga mkono serikali ya mpito chini ya Hamdok na wale wanaotaka jeshi kuchukua uongozi wa nchi hiyo.
Serikali ya mpito inayoundwa kati ya raia na Baraza la kijeshi iliundwa mwaka 2019 baada ya kuangushwa kwa utawala wa kiongozi wa muda mlrefu Omar Al Bashir kufuatia maandamano ya wananchi, na ilipaswa kuongoza mpaka 2023 na kupisha Uchaguzi Mkuu.