Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 3:41 pm

NEWS: JESHI LA SUDAN LASITISHA MAZUNGUMZO NA WAANDAMANAJI

Jeshi la Sudani kupitia kiongozi wake Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ametangaza kusitisha mazungumzo na viongozi wa waandamanaji kwa saa 72, wakati huu waaandamanaji wakiendelea kusisitiza hawataacha kupiga kambi nje ya makao makuu ya jeshi.

Related image

Watu 14 wamejeruhiwa kwa risasi nchini Sudan baada ya jeshi kujaribu kuwaondoa waandamanaji waliopiga kambi nje ya makao makuu ya jeshi jijini Khartoum.

Makabiliano haya yameshuhudiwa saa chache baada ya jeshi na viongozi wa waandamanaji kukubaliana kuunda serikali ya mpito itakayodumu kwa muda wa miaka mitatu.

“Kulikuwa na watu ambao walikuwa na nia mbaya kati ya wanadamanaji waliowalenga maafsa wetu wa usalama,” amesema Jenerali Burhan.

Hata hivyo, waandamanaji wanawalaumu wanajeshi kwa kuwashambulia, kauli ambayo pia imeungwa mkono na Balozi wa Uingereza nchini humo Irfan Siddiq.

Kupitia katika ukurasa wake wa Twitter, Siddiq amesema anasikitishwa kuona jeshi likitumia risasi kuwashambulia waandamanaji.

Kabla ya kusitishwa kwa mazungumzo hayo, wanajeshi na waandamanaji walikuwa wamekubaliana kuunda serikali ya mpito kwa muda wa miaka mitatu.