November 26, 2024, 6:30 pm
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JESHI LA SUDAN LAPIGA MARUFUKU BENKI KUU KUHAMISHA FEDHA
Baraza la Kijeshi nchini Sudan lililompindua Rais Omar Al- Bashiru, ambalo ndilo linaloongoza serikali ya mpito la nchi hiyo, limeiamuru Benki Kuu ya nchi hiyo, kuchunguza mara moja shughuli zote za uhamishaji wa fedha zilizofanyika kuanzia Aprili 1mwaka huu, na kushikilia fedha zote zinazotiliwa shaka.
Taarifa Hiyoimeripotiwa leo Alhamisi na shirika la habari la Sudan, SUNA. Baraza hilo pia limeamuru kusimamishwa kwa shughuli ya kubadilishwa umiliki wa hisa, hadi itakapotangazwa vinginevyo. Benki Kuu vile vile imeamuliwa kuripoti kwa mamlaka husika, juu ya kufanyika mchakato wowote wa uhamishaji mkubwa, au unaotiliwa shaka ya hisa pamoja na umiliki wa makampuni.