Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 7:37 am

NEWS: JESHI LA SUDAN LAGAWANA MADARAKA NA VIONGOZI WA MAANDAMANO

Wawakilishi wa utawala wa kijeshi na viongozi wa waandamano nchini Sudan wametia sahihi "tamko la kisiasa" la kugawana madaraka katika kipindi cha mpito, baada ya Omar al-Bashir kutimuliwa madarakani mwezi Aprili, waandishi wa habari wa shirika la Habari la AFP wamebaini.

media

Mazungumzo bado yatafanyika katika siku zijazo kuhusu pointi nyingine zinazoendelea kuzua mgongano kwenye makubaliano yaliyofikiwa Julai 5 kati ya pande mbilii, kulingana na wawilishi wa waandamanaji.

"Tamko la kisiasa" limetiliwa saini na pande mbili baada ya mazungumzo marefu usiku wa Jumanne kuamkia leo Jumatano.

Baada ya mkutano katika hoteli moja ya kifahari jijini Khartoum, kiongozi namba 2 wa Barazala Kijeshi, Mohamed Hamdan Daglo kwa jina maarufu "Hemeidti", pia Mkuu wa kikosi cha kupambana na fujo (RSF), amepongeza hatua hiyo akiita ni ya "kihistoria ".

"Leo tumekubaliana kuhusu tamko la kisiasa," Ibrahim al-Amin, mmoja wa viongozi wa maandamano, ameliambia shirika la Habari la AFP. "Kuhusu nakala ya katiba, tutaanza tena mazungumzo siku ya Ijumaa," amesema.

Mkataba huu ni hatua ya kwanza kuelekea serikali ya kiraia, iliyoombwa na wananchi wengi wa Sudan kwa karibu miezi saba.