Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 2:47 pm

NEWS: JESHI LA SUDAN LAAGIZA KUFUGWA KITUO CHA TELEVISHENI CHA ALJAZEERA

Mamlaka za kijeshi nchini Sudan zimekitaka kituo cha habari cha Aljazeera kufunga ofisi zake mara moja mjini Khartoum kwa maelekezo ya baraza kuu la kijeshi, bila hata ya kutoa sababu yeyote.

Image result for aljazeera in sudan office

Uamuzi huu wa jeshi unamaanisha pia kunyang'anywa vibali vya kufanyia kazi nchini humo kwa wawakilishi wa kituo hicho pamoja na wafanyakazi wengine.

Kwa miezi kadhaa sasa waandamanaji wameendelea kutia ngumu kutoka kwenye maeneo yanayozingira makao makuu ya jeshi wakishinikiza jeshi kukabidhi madaraka kwa utawala wa kiraia.

Katika taarifa yake uongozi wa Aljazeera umekashifu hatua ya baraza la kijeshi, wakisema kitendo hiki ni ukiukaji mkubwa wa uhuru wa watu kutoa na kupata habari.

Utawala huo wa kijeshi unasema kuwa kambi za waandamanaji mjini Khartoum zimekuwa tishio kwa usalama wa taifa

Image result for aljazeera in sudan office

"Eneo la maandamano limekuwa si salama na linahatarisha usalama wa taifa," alisema Jenerali Bahar Ahmed Bahar, mkuu wa jeshi mjini Khartoum.

Jeshi linasema magari maalumu ya kijeshi ya kikosi maalumu yamekuwa yakishambuliwa na mengine kuzuiliwa na waandamanaji kwenye eneo la maandamano.

Eneo hilo limekuwa kitovu cha vuguvugu la maandamano, ambayo yalishuhudia kuondoka madarakabi kwa rais Omar al-Bashir aliyeondolewa na jeshi mwezi uliopita, na tangu wakati huo wamekuwa wakitaka wanajeshi nao kukabidhi madaraka kwa raia.