- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JESHI LA POLISI MWANZA LINAWASHIKILIA WATUHUMIWA 56 WA UHALIFU
Mwanza: Jeshi la polisi mkoani Mwanza linawashikilia watuhumiwa 56 wa matukio mbalimbali wakiwamo wahamiaji haramu na waganga wa kienyeji wanaojihusisha na ramli chonganishi katika Jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake, kamanda wa polisi mkoa huo, Jumanne Murilo amesema katika tukio la kwanza wamekamata wahamiaji haramu 19 raia wa Ethiopia waliokutwa nyumba ya kupanga mtaa wa Amani kata ya Butimba jijini Mwanza.
Amesema watuhumiwa hao walikamatwa jana saa 5.00 asubuhi kwenye chumba alichopanga mkazi wa mtaa wa Mkuyuni ikiwa ni siku tatu toka achukue chumba hicho. "Jeshi la polisi linaendelea kuwashikilia na watafikishwa katika idara ya uhamiaji kwa ajili ya hatua nyingine za kisheria," amesema Muliro.
Katika tukio jingine, polisi wamewakamata waganga wa kienyeji 15 wanaopiga ramli chonganishi, kati yao wakiume sita na wa kike 10 wakiwa na nyara za Serikali. Kamanda Muliro alizitaja nyara hizo kuwa ni, mikia miwili ya nyumbu, magamba ya chatu, vipande vya mayai ya mbuni, pembe za wanyamapori, mafuta ya simba, ngozi ya kenge na vipande vinne vya ngozi vya wanyamapori aina tofauti