Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 1:55 am

NEWS: JESHI LA POLISI MWANZA LIMEDHIBITISHA KUWASHIKILIA WASAIDIZI WA MNYIKA

Mwanza. Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza liliwashikilia na kuwafanyia mahojiano wasaidizi wawili wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro amewataja leo Desemba 30, 2019 kuwa walioshikiliwa, na kuwekwa mahabusu na baadae kuachiwa baada ya mahojiano kuwa ni Ofisa Habari wa Chadema na Msaidizi binafsi wa Mnyika, Abdulkarim Muro pamoja na dereva wa Katibu Mkuu huyo, Said Haidan.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Kamanda Muliro amesema watu hao walikamatwa kwenye nyumba moja iliyo karibu na hoteli ya Paradise eneo la Mahina jijini Mwanza baada ya Polisi kupata taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu kuwepo kwa watu wanaotiliwa mashaka kuwa ni wahalifu.

Jana Uongozi wa Chama hicho Ulitoa taatifa kupitia mtandao wa twitter kwa umma juu ya Kukamatwa kwa Wasaidizi hao wa katibu mkuu wa chama hicho