Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 11:39 pm

NEWS: JESHI LA POLISI MKOANI TANGA LAKAMATA GRAMU 187 ZA DHAHABU

Tanga: Taarifa kutoka mkoani tanga zinaripoti kuwa Jeshi la Polisi Mkoani humo zimekamata zaidi ya Gramu 187 za dhahabu zinazokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya Sh13 milioni

Image result for Godwin Gondwe na jeshi la polisi

Dhahabu hizo zimekamatwa na kamati ya ulinzi na usalama wilayani handeni katika mgodi wa dhahabu wa Magambazi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Machi 21, 2019 , Mkuu wa wilaya ya Handeni ambaye pia ndio mwenyekiti wa kamati hiyo, Godwin Gondwe amesema wahusika walifanya uchenjuaji madini hayo bila kufuata taratibu za kisheria.

Gondwe amesema Jeshi la Polisi linamshikilia mkuu wa kambi ya machimbo ya dhahabu ya Magambazi kwa tuhuma ya kushindwa kutoa taarifa kwenye vyombo husika wakati uchenjuaji dhahabu ukifanyika licha ya kufahamu taratibu. “Hii ni dalili ya kutaka kutorosha madini haya.

Kaimu ofisa madini mkazi mkoa wa Tanga, Nicas Sangaya amesema walipata taarifa madini hayo yanataka kutoroshwa na baada ya kufuatilia walibaini ni kweli. “Thamani ya madini haya ni zaidi ya Sh13 milioni, ni gramu 186.9. Tutayachukua madini haya na kuyapeleka ofisi za Benki Kuu (BoT) tawi la Arusha kwa ajili ya kuhifadhiwa kama taratibu zinavyoelekeza,” amesema Sangaya.

Taratibu za madini zinaeleza wazi kuwa wakati wa uchenjuaji katika hatua za mwisho wanatakiwa kuishirikisha kamati ya ulinzi na usalama lakini hawakufanya hivyo,” amesema Gondwe.