- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA MKURUGENZI WA ITIGI KWA MAUWAJI
Watu watano, akiwamo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi, Pius Luhende, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Singida, wakituhumiwa kusababisha kifo cha mfugaji Peter Chambalo, anayedaiwa kupigwa risasi akiwa kanisani.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Ahmed Msangi, alikiri kutokea kwa tukio hilo juzi na kueleza kuwa mpaka sasa, wanaoshikiliwa ni watu wa watano akiwamo mkurugenzi huyo.
Msangi alitaja watuhumiwa wengine wanaoshikiliwa kuwa ni askari wanyamapori wawili, mmoja kutoka Mamlaka ya Wanyamapori (Tawa) na mwingine kutoka Halmashauri ya Itigi, mwanasheria na mtendaji wa kata.
“Ni kweli tukio limetokea, lakini siyo kweli kuwa askari wa Jeshi la Polisi wamehusika na tukio hilo," Msangi alisema, "kwanza hawakuwapo kwenye tukio hili. "Waliokuwapo ni askari wanyamapori, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi, mwanasheria wake na mtendaji wa kata. Kilichotokea ni kwamba, walipofika katika kijiji cha Kazikazi, Kata ya Kitaraka, Tarafa ya Itigi, kulitokea kutoelewana, hivyo kusababisha vurugu," alisema. Aliongeza kuwa, wakati wa vurugu hizo, inadaiwa askari walifyatua risasi na kumjeruhi mtu huyo ambaye alifariki dunia. “Uchunguzi wa tukio hili unaendelea na hivi sasa Mkuu wa Mkoa huo, Kamanda wa Polisi wapo eneo la tukio kupata maelezo zaidi, hizi ndizo taarifa nilizonazo hadi sasa,” Msangi alisema.