- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JESHI LA POLISI LAZUIA MKUTANO WA CUF TABORA
Tabora. Jeshi la polisi Mkoani Tabora limezuia kongamano la Chama cha Wananchi (CUF) lililokuwa limepangwa kufanyika leo Jumatano Oktoba 9, 2019 Wilaya ya Tabora kwa minajili ya kuhamasisha uandikishaji wa wapiga kura kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019.
Mbali na kuzuia kongamano hilo, pia wamezuia ufunguzi wa matawi ya chama hicho wilayani humo uliokuwa ufanyike kesho Alhamisi.
Kongamano hilo ni mwendelezo wa ziara ya mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba kuimarisha chama hicho na kuhamasisha uandikishaji wa wapiga kura kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019.
Jana Jumanne Oktoba 8, 2019 kamanda wa polisi Wilaya ya Tabora alikiandikia barua chama hicho akikitaka kutofanya shughuli hizo.
Barua hiyo inaeleza kuwa kutokana na tathmini ya hali ya ulinzi na usalama kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa katika jamii kuna mihemko ya kisiasa inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani.
"Kwa mazingira hayo na kwa nia njema yakuendeleza amani na utulivu bado mikutano ya nje ya kisiasa hairuhusiwi kwa kipindi hiki na hatuna pingamizi na mikutano ya ndani,β inaeleza sehemu ya barua hiyo.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Tabora, Barnabas Mwakalukwa amesema polisi haijazuia mikutano ya ndani ila kilichozuiwa ni ufunguzi wa matawi.
"Mkishakusanyika zaidi ya mmoja tayari ni mkutano wa hadhara ufunguzi wa matawi unakuwa na shamrashamra ila wakikaa kikao cha ndani sina shida,β amesema Mwakalukwa
Kwa upande wa CUF Mkurugenzi wa habari na mahusiano ya umma wa Chama hicho, Abdul Kambaya amesema kinachofanyika si mkutano wa hadhara bali ni ufunguzi wa matawi, kongamano hilo litafanyika kwenye ukumbi, si sehemu ya wazi.