- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JESHI LA POLISI LAVAMIA MKUTANO MKUU WA ACT WAZALENDO
Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam limevamia Mkutano wa Ndani wa viongozi na wanachama wa chama cha ACT Wazalendo na kisha kuwatawanya wanachama Hao katika Ukumbi wa Mikutano wa PR Stadium (Karibu na Uwanja wa Taifa wa Mpira Jijini Dar es Salaam),
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi wanasema kuwa wamefanya hivyo kutokana na intelejensia yao kuonesha kuwa huenda mkutano huo unaweza ukagubikwa na kutokea vurugu za wanachama wa chama cha wananchi CUF kuvamia ndani ya Mkutano huo.
Wanachama wengi wamehoji hatua ya jeshi hilo kuvamia mkutano huo, muakilishi Media tumepiga stori na mmoja wa mwanachama wa chama hicho Jumanne Mpolali yeye anasema kuwa ''kama hoja ni sisi kuvamiwa na hao wanachama wa chama kingine ndio polisi wanatakiwa kutupatia ulinzi wa kutosha kuhakikisha tuko salama na mkutano wetu unaenda kama tulivyopanga, kwa sababu kazi ya polisi ni kulinda Raia na mali zao, sasa mi nahisi hawana lengo zuri hata kidogo, mi ushauri wangu kwa mamlaka za juu na jeshi la polisi watende haki kwa wanachi wote" amesema mwanachama huyo
Jana Kiongozi wa Chama hicho ambae pia ni Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe kwa kushauriana na Kamati ya Uongozi ya Chama kufuatana na kifungu cha 29 (25)(v) cha Katiba ya Chama hicho alimteuwa Ndugu Juma Duni Haji kuwa Naibu Kiongozi ya Chama cha ACT Wazalendo. Uteuzi huo umeanza rasmi leo tarehe 27 Machi 2019.
Chama hicho kwa sasa kinakabiliwa na hati hati ya kufutiliwa mbali na msajili wa vyama vya siasa nchini kwa kile kinacho daiwa kuwa chama hicho kuvunja sheria ya vyama vya siasa nchini, madai ambayo kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe alizijibu.