- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JESHI LA POLISI KUTOLEA MAELEZO KESHO WAPI ALIPO TITO MAGOTI
Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema atolitolea ufafanuzi kesho Jumatatu Desemba 23, 2019 swala la kumshikilia Ofisa wa Kitengo cha Elimu kwa Umma wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Tito Magoti.
Magoti alikamatwa na polisi Ijumaa Desemba 20 eneo la Mwenge, Dar es Salaam tukio lililozua mjadala kwenye mitandao ya kijamii ikidaiwa kuwa ametekwa.
Hata hivyo, siku hiyo jioni polisi walieleza kuwa Magoti (26) hajatekwa na wanamshikilia pamoja na wenzake licha ya kutoweka wazi wapo kituo gani cha polisi.
Akizungumza na MuakilishiTZ leo ASUBUHI Jumapili Desemba 22, 2019 Mambosasa amesema,"Huyu kijana yupo mikono salama pamoja na wenzake watatu na yupo katika kituo cha polisi hatuonyeshi mtu yoyote, hebu subiri taarifa itatolewa kesho mbele ya waandishi wa habari. sawa”