- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JESHI LA POLISI KILIMANJARO LASITISHA MKUTANO WA FREEMAN MBOWE
Jeshi la polisi wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro limesitisha mikutano ya hadhara iliyokuwa imepangwa kufanywa na Mbunge wa Jimbo la Hai Freeman Mbowe kwa madai ya kiusalama kwasababu Mkuu wa wilaya hiyo Lengai Ole Sabaya atakuwa na ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi
Kwa mujibu wa barua iliyotolewa na Lwelwe Mpina, Mkuu wa Jeshi la Polisi Hai leo tarehe 29 Julai 2019, Jeshi hilo limesitisha mikutano hiyo hadi pale Ole Sabaya atakapomaliza ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi.
“Kutokana na ufinyu wa nguvu kazi. Hivyo kwa busara sisitisha ziara na mikutano unayotegemea kuifanya hadi Mhe. Mkuu wa Wilaya atakapomaliza ziara yake,” inaeleza barua hiyo.
Barua hiyo inaeleza kuwa, kama Mbowe na Sabaya wote wakifanya mikutano, kutatokea muingiliano wa mikutano na ziara, na kusababisha uvunjifu wa amani ambao utahatarisha usalama wa wananchi.
“Napenda kukutaarifu kuwa Mkuu wa Wilaya Mhe. Lengai Ole Sabaya ana ziara wilayani hapa tangu 24/7/2019 kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi. “Hivyo, kwasababu za kiusalama, kuingiliana kwa mikutano na ziara kunaweza kusababisha uvunjifu wa amani ambao utahatarisha usalama wa wananchi,” inaeleza barua hiyo.,
Hata hivyo, Basil Lema ambaye ni Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, amesema mikutano ya hadhara ya Mbowe, imeahirishwa baada ya kufiwa na kaka yake, Alfred. Alfred amefariki dunia jana tarehe 28 Julai 2019 ikiwa ni siku moja kabla ya Mbowe kuanza ziara ya mikutano ya hadhara kwenye jimbo lake la Hai mpaka tarehe 1 Agosti 2019.