- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JESHI LA POLISI KIGOMA LIMEWAUWA MAJAMBAZI 12
Kigoma: Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limewaua watu 12 wakishukiwa kuwa ni majambazi waliodaiwa kuwa katika mpango wa kuteka magari katika kijiji cha Kilemba wilayani Kibondo mkoani humo
Akizungumzia jana Ijumaa Septemba 13, 2019 Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, Martin Otieno amesema siku za hivi karibuni kumeibuka matukio ya utekaji magari, baadhi ya waliokamatwa walieleza matukio hayo.
Amesema polisi walifika eneo hilo na kuanza kurushiana risasi na watu hao na kuwaua 12 waliokutwa na bunduki tatu aina ya AK 47, risasi 107, mapanga, visu na mabomu matatu ya kurusha kwa mkono.
‘’Licha ya kuwa wananchi wa Burundi wanajihusisha na ujambazi, hapa nchini natoa onyo kwa Watanzania wanaowakaribisha watu hawa ukibainika utachukuliwa hatua.”
“Wengi wamegeuza mkoa wa Kigoma kuwa sehemu salama kwao kwa kufanya mambo yao yasiyofaa sasa tutamshughulikia kila mtu ambaye hataki kufuata sheria za nchi yetu awe mgeni au mwenyeji,” amesema Otieno.