- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JESHI LA MAGEREZA LAAHIDI KUANZA KUJITEGEMEA
Dodoma. Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Tanzania, Kamishna Jenerali Suleiman Mzee amesema kuanzia mwezi Machi Mosi, mwaka huu Magereza zote nchini Tanzania zitaanza kujitegemea kwa asilimia mia moja kwa chakula cha wafungwa na huduma nyinginezo zote.
Mzee ametoa kauli hiyo leo Jumatano Februari 19, 2020 mjini Dodoma katika kikao kazi cha maofisa waandamizi wa jeshi hilo kutoka mikoa yote Tanzania Bara kwa ajili ya kupeana mikakati ya namna ya kufanikisha mpango wa kujitegemea.
Amesema uamuzi huo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Tanzania, John Magufuli ambaye mara kadhaa amekuwa akiagiza Magereza nchini kujitegemea kwa kuwatumia wafungwa kufanya shughuli mbalimbali za kilimo
“Magereza kujitegemea inawezekana kwani tunazo rasilimali nyingi ikiwemo mashamba ya kilimo, mifugo, wataalam wa kutosha na nguvu kazi ya wafungwa. Tukisimamia vizuri na kuachana na ubinafsi tutaliwezesha jeshi letu kujitegemea,” amesema Kamishna Jenerali Mzee.
Amewataka wakuu wote wa Magereza kuhakikisha wanaanza kujitegemea, “kuanzia Machi Mosi kila mkuu wa magereza ahakikishe anajitegemea katika mkoa wake na lazima mkubali kufanya mabadiliko haya bila visingizio. Atakayeshindwa kujitegemea nitamwajibisha mara moja.”
Amebainisha kuwa tayari ameanza maandalizi ya ujenzi wa ofisi za makao makuu ya jeshi hilo pamoja na nyumba za watumishi jijini Dodoma kwa kutumia rasilimali mbalimbali.
Kikao kazi cha maofisa waandamizi wa Magereza ndio kikao cha juu cha uongozi kinachowakutanisha maofisa waandamizi kutoka makao makuu, wakuu wa magereza wa mikoa, mkuu wa kikosi maalum ,mkuu wa Sekondari Bwawani na wakuu wa vyuo.