Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 5:30 pm

NEWS: JE NANI MUONGO BAINA YA CAG NA WAZIRI LUGOLA

Dodoma: Jana Jumatano April 25 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola ameushutua umma baada ya kutoa taatifa yake bungeni kuwa Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serekali (CAG) Prof. Mussa Assad kuwa ni mtu muongo kwa kuwasilisha taarifa kwa Rais ikionesha kuwa Jeshi hilo la Polisi lilipokea sara hewa zilizongharimu Sh. bilioni 16 za Jeshi hilo.

"Hakuna mtu muongo kama CAG na nikotayari kuweka uwaziri wangu rehani, ikiwa itabainika kuwa taarifa zake za ukaguzi kuhusu sare hewa za jeshi la polisi zilizogharimu Sh16bilioni ni ya kweli"


Sasa Ripoti ya CAG Kurasa No.310 Inasema Kukosekana kwa nyaraka za kuthibitisha uletaji wa mzigo. Niliomba Hati ya kupokelea Shehena ya Mzigo Bandarini (Bill of Lading), Hati ya Madai kutoka kwa Mtengenezaji (Commercial Invoice),

Hati ya Mzigo ulipotoka (Certificate of Origin), orodha za mali zilizopo kwenye meli (Packing List) na cheti cha ukaguzi wa bidhaa (Inspection Certificate) kutoka kwa Mzabuni Daissy General Traders kwa ajili ya kujiridhisha kama bidhaa husika zililetwa nchini.

Hata hivyo Mzabuni alishindwa kuwasilisha nyaraka hizo. Aidha, nilipitia Mfumo wa Forodha (TANCIS) wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na kubaini kuwa hapakuwa na shehena yoyote kutoka kwa Mzabuni Daissy General Traders mwezi Novemba 2015.

Ukienda mpaka kipenge d) nilifanya mahojiano na Maofisa wa Bohari kuu ya Jeshi la Polisi na kubaini hakukuwa na Sare zozote zilizoletwa na Mzabuni Daisy General Traders mwezi Novemba 2015. Hivyo, Serikali imepata hasara kubwa kwa kufanya malipo ya Sare za Polisi ambazo hazikuletwa na Mzabuni.

Baada ya Maelezo hayo CAG alitoa Ushauri Kuhusu suala hili, "nashauri Mzabuni Daissy General Traders arejeshe kiasi alicholipwa kwa kutoleta Sare za Polisi na hatua stahiki za kinidhamu na kisheria zichukuliwe kwa Maofisa wote wa Jeshi la Polisi kwa kuisababishia Serikali hasara. "