Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 11:38 pm

NEWS: JAMHURI YASEMA KESI YA KABENDERA UPELELEZI BADO KIDUCHU

Upande wa mashtaka (Jamhuri) katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwandishi wa habari za uchunguzi nchini Tanzania Erick Kabendera, umeielezea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi katika kesi hiyo umebakia katika maeneo machache kukamilika.

Wakili wa serikali, Easter Martin ameyaeleza hayo leo Januari 13, mwaka 2020 wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janet Mtea

"Mheshimiwa kesi leo imekuja kwa ajili ya kutajwa upelelezi bado haujakamilika ila tuko katika hatua za mwisho, bado maeneo machache ili kukamilisha,"amedau.

Hata hivyo hakimu Mtega ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 27,mwaka 2020 na mshtakiwa Kabendera amerudishwa rumande.

Katika tarehe iliyopita, upande wa mashtaka alieleza Mahakama kuwa, mwenendo wa kesi, upelelezi unaendelea na shauri limefikia hatua nzuri ya maelewano baina ya mshitakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka (DPP).

Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa Sh.Mil 173. Inadaiwa katika kipindi hicho, Kabendera alijihusisha na mtandao wa kihalifu kwa kutoa msaada kwa genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.

Pia inadaiwa katika kipindi hicho, bila ya sababu,alikwepa kodi ya Sh.173,247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).