November 26, 2024, 9:14 pm
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JAMBAZI AFARIKI DUNIA KWA KUPIGA RISASI NA JESHI LA POLISI
SONGWE: Jeshi la polisi mkoa wa Songwe limekabiliana na watu wanne wanaosadikika kuwa majambazi waliokuwa tayari kutekeleza tukio la uharifu nyumbani kwa mfanyabiashara mmoja mkazi wa mji wa Viwawa wilayani Mbozi, ambapo katika majibizano makali ya risasi askari polisi wamejeruhiwa huku jambazi mmoja ambaye akifariki njiani wakati akiwahishwa hospitali na baada ya kupekekuliwa amekutwa na silaha tatu zikiwemo bunduki yenye risasi na kifaa maalum cha kuzimisha faham kijulikanacho kama taser huku majambazi wenzake watatu wakitokomea kusiko julikana.
Kamishna msaidizi wa jeshi la polisi kamanda wa polisi mkoa wa Songwe Mathius Nyange amesema baada ya kumpekua jambazi aliyejeruhiwa wamemkuta na silaha tatu ikiwemo bunduki na risasi 3, upanga na kifaa cha kisasa kinachotumika kumzimisha mtu fahamu wakati wa kufanya tukio, hata hivyo jambazi huyo amefariki dunia kutokana na majeraha ya risasi.
Kufuatia tukio hilo wakazi wa mkoa wa Songwe wameshauri jeshi la polisi kuhakikisha usalama wa raia wanaothubutu kutoa taarifa kwa jeshi la polisi zinazohusu wahalifu na kusisitiza elimu ya polisi jamii na ulinzi shirikishi iimarishwe ili wananchi washiriki ipasavyo kutokomeza matukio ya uhalifu.
Aidha kamanda Nyange amesema mkoa wa Songwe sio mahali salama kwa watu wanofanya uhalifu na kuongeza kuwa wakija hawatarudi salama.