- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JAJI MWANZA AAGIZA MAHABUSU MWANZA KUACHILIWA HURU
Katika hali isiyo ya Kawaida Jaji mfawidhi wa mahakama kuu nchini Tanzania, Kanda ya Mwanza, amewataka mahakimu mkoani humo kuepuka kwa kiwango kikubwa kutoa adhabu ya kifungo ikiwa ni sehemu ya kupambana na maambukizi ya Corona.
Katika barua iliyoandikwa kwa mahakama za hakimu mkazi na mahakama za wilaya mkoani humo, Jaji SM Rumanyika amewataka mahakimu kutoa adhabu mbadala na kutaka makossa yote yenye dhamana washtakiwa waachiwe kwa dhamana
"Utaona kwa vyovyote vile maelekezo haya yanakinzana nataratibu, mazoea na labda kwa kiasi Fulani sheria. Fahamuni kuwa maisha ya watu wengine na maisha yetu ni bora zaidi", amesema Jaji Rumanyika
Baadhi ya wanasheria wamefurahishwa na agizo la Jaji Rumanyika,
"Hongera Mh. Jaji Rumanyika! Utendaji unapaswa kuwa kama hivi", ameandika Anna Henga, wakili na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
Ameleekeza pia kwamba, pamoja na uweka maji yanayotiririka yenye dawa na sabuni, ni washtakiwa, mashahidi, warufani/warufaniwa na au mawakili wao tu ndio watakao ruhusiwa kuingia katika kumbi na chemba za mahakama